Wednesday, May 11, 2016

Kutana na Mkongwe wa Reggae Tanzania Jailany a.k.a "Babu Rasta wa Roots & Kalcha" !!!



Kutana na Muimbaji mkongwe wa mziki wa Reggae kutoka “ Jailany Group”, Ahmed Abdul Ramole a.k.a Rasta, a.k.a Jailany a.k.a babu Rasta. Jailany, muanzilishi na mmiliki wa Roots and Kalcha Coop Ltd ambaye pia ni mmiliki wa Jailany Group (1964) ni msanii mkongwe aliyeleta mabadiliko makubwa sana kwenye Tasnia ya mziki nchini Tanzania hususani mziki wa Reggae/ Sweet Reggae.




Ahmeds son Jamaal and wife, Meryl Franco
Jailany ameoa na ana watoto watano, Jamaal, Gibran, Fatna, Miriam na Asha.Jailany ameshawahi kufanya kazi na Bendi nyingi maarufu hapa nchini zikiwemo Skyblues (1963) ambapo alifanya kazi kiukaribu na wasanii kama Erick Wamba, Andrew Hamigo (who now lives in London) na wengine wengi, pamoja na Bendi ya “OS Africa Jazz” (1972), bendi iliyomilikiwa na bw.Pascal Onema.



 Akiwa ndani ya bendi ya OAJ, Jailany anasema aliweza kufanya kazi kwaukaribu na Papa Mickey na wasanii wengine wakongwe ambao kwa njia moja ama nyingine wasanii hawa walimsaidia kufika katika level ingine.



 Mwaka 1964 Jailany aliiaga bendi hiyo ya OAJ na kuanzisha bendi yake binafsi  ya “Jailany Group”. Bendi hii ilifanya vizuri sana na kupelekea kushinda Tuzo kadha wa kadha ikiwemo tuzo ya Bendi Bora ya mwaka 1965.Bendi hii imewatoa wasanii wengi maarufu wa sasa akiwemo Jado FieldForce, Badi Bakule (Twanga Pepeta),marehemu Muscho Kombo ,Muscho Kombo (the late), Bwamy Fanfan, Rama Issa (Key board), Rashid Kalala, Juma Mikulandi (Drummer) na wengine wengi.


Son, Gibran
with his daughters Fatna &Asha
Mnamo Mwaka 1972, Jailany aliamua kuchukua mapumziko mafupi kwenye bendi hiyo nakuelekea nchini Canada kuongeza elimu yake katika chuo cha Winnipeg (Winnipeg University) ambapo alihitimu Shahada ya kwanza (BA Economics) na baadaye akaenda Chuo cha Manitoba kwa ajili yakuchua Shahada ya Uzamili (Masters in Public Admin) kabla ya kumalizia shahada ya uzamivu chuoni hapo.
Ahmeds wife(Fatma) & son (Jamaal)
Ahmed with wife & daughter

Best Friends son, Jazhindo
Daughter,Miriam
 Fatna,Jamaal and his wife Meryl
(Son & Daughter) Jamaal & Fatna 

No comments:

Post a Comment