![]() |
Watangazaji wa Azam TV (kutoka kushoto) ni Raymond
Nyamwihula, Zainab Chondo, Rehema Salum, Nurdin Suleiman, Fatuma Almasi
Nyangasa, Baruani Muhuza, Ivona Kamuntu na Charles Hilary.
|
Kuanzia leo taarifa ya habari ya Azam TV itakuwa
ikisomwa na watangazaji wawili na kutakuwa na pea tatu tofauti za watangazaji.Kuanzia leo taarifa ya habari ya Azam TV itakuwa
ikisomwa na watangazaji wawili na kutakuwa na pea tatu tofauti za watangazaji.
![]() |
Tido Mhando (Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Televisheni) |
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Televisheni, Tido Mhando
alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wamejiandaa vilivyo kuhakikisha kuwa
mbali na studio bora wanakuwa pia na kikosi cha wanahabari wenye uwezo mkubwa.
Tido aliwataja baadhi ya waandishi na watangazaji
ambao wameungana na Azam TV kuwa ni Charles Hilary, Baruani Muhuza, Ivona
Kamuntu na Fatuma Almasi Nyangasa.
“Watangazaji hao sasa wataungana na wasomaji wetu
wazuri wa siku nyingi Rehema Salum na Nurdin Suleiman kukamilisha pea tatu za
wasomaji wa mtindo wa wawili wawili,” alifafanua Tido.
Tido alisema leo na kesho habari itasomwa na Charles
Hillary na Ivona Kamuntu wakati siku mbili nyingine itakuwa ni zamu ya Baruhani
Muhuza na Fatuma Nyangasa huku Rehema Salum na Nurdin Suleiman nao wakiwa na
zamu yao.
Alisema licha ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku
pia wanatarajia hivi karibuni kuanzisha taarifa ya habari ya saa saba mchana
itakayokuwa ikiendeshwa na Zainab Chondo na Raymond Nyamwihula.
“Mpango wote huu wa mabadiliko haya ya utangazaji na
upatikanaji wa habari wa Azam TV utakuwa unasimamiwa na kuratibiwa na Joseph
Warungu aliyekuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza kitengo cha BBC cha Focus on
Africa,” alisema Tido.
Source: Mwananchi
No comments:
Post a Comment