Thursday, August 13, 2015

Nisha Akanusha Kukamatwa na Madawa Ya Kulevya !!!



Siku hizi mwanamke yeyote mzuri/ maarufu akivuka Border ni muuza unga. Baada ya Jacky Patrick kukamatwa na madawa ya kulevya mnamo  Mwezi December 2013 huko Macao China.

Hivi karibuni ,msanii kutoka Tollywood, Nisha Jabu amekuwa akipost picha nzuri kweli akila starehe nchini China. Kwa kuwa inasemekana ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo watu wakaanza kufuatilia kutaka kujua kunani ? WaTanzania ni wapekuzi sana jamani, khaa ! ... Bofya hapa kwa stori kamili ...

 Baada ya tetesi kusambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa msanii wa Filamu nchini Tanzania, Salma Jabu al maarufu kama "Nisha", amekamatwa nchini China, kutokana na kukutwa na madawa ya kulevya, mrembo huyo amekanusha tetesi hizo nakudai kuwa habari hizo sii za kweli.



Kupitia mtandao wa kijamii amebainisha tuhuma hizo na kuandika “Ok naomba leo niweke wazi hili swala lililoandikwa na kusambaa kuwa nimekamatwa China na madawa,hii ni kwa mashabiki zangu (huwa napenda kupuuzia vitu ila wacha niongee leo ili nisiwape watu presha na maswali mengi na kuwaweka njia panda)mimi sijakamatwa,sijawahi kukamatwa na wala sitaweza kukamatwa kwa ajili ya ujinga kama huo wa madawa ya kulevya
1)siyapendi
2)hata niwe maskini vipi siwezi kujiingiza kwenye janga hilo,”.


“Kilichotokea nihiki, kutokana na WaTanzania kuharibu sana na scandals za kukamatwa na madawa ya kulevya, (wengi mnalijua hilo) ukiwa unavuka border ukionekana tu passport yako ni ya Tanzania basi unaserchiwa sana,of course yeah waliniserch all most 3/4 hrs.. hilo kwa WaTanzania wanaovuka kwenda Hong Kong n.k nadhani mmenielewa. . Si mimi tuu mTanzania yyte au wanigeria au utaifa wwte wenye history ya nchi yao kukamatwa kwa unga lazma shughuli ikupate.. Hawajanikuta na kitu I’m ok.. na nna visa yao ya muda mrefu tu.. laiti ukikamatwa na madawa my dear nchi hizi unaozea jela,na sasa yangeongeleka mengine.. pls msiniombee mabaya hayo basi.. Nb:Global publishers waliandika ukweli.. sasa sijui hiyo blog nyingine ilojitokeza na kuandika uongo ilikusudia nn.. All n all #nawapenda wote,”. Alindika Nisha




No comments:

Post a Comment