Monday, August 17, 2015

Nancy, Mshindi wa Tuzo Ya Komla Dumor !!!

Mwanahabari kutoka Uganda, Nancy Kacungira ni mshindi wa Tuzo ya kwanza ya kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC, Komla Dumor.


Tuzo hiyo ya BBC World News Komla Dumor Award, ina lengo la kuendelea kuimarisha uandishi wa habari kuhusu Afrika.


Mtangazaji huyu wa kituo cha televisheni cha KTN cha Kenya,alichaguliwa miongoni mwa washiriki wapatao 200.

Mshindi huyo atakuwa makao makuu ya BBC, mjini London kwa miezi mitatu na pia kutuma taarifa za habari za BBC Televisheni , radio na mtandaoni kutoka barani Afrika.


 Tuzo hii ilianzishwa ili kumuenzi Komla Dumor, mtangazaji wa BBC, aliyeaga dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 41.


Bi Kacungira alisema: " nimeshtushwa, lakini pia kufurahishwa sana kwa kupokea habari hii.

Nimepokea kwa unyenyekevu mkubwa ushindi wa tuzo hii".


No comments:

Post a Comment