Ali Kiba na Neyo
walijumuika pamoja na wasanii wengine wa Africa wakiwemo Wangechi (Kenya) Dama Do Bling (Mozambique), Ice
Prince(Nigeria) pamoja na Maurice Kirya
(Uganda).
Wasanii hawa watarekodi wimbo wa pamoja, msimu mpya
wa “Coke Studio Africa” ambao utazinduliwa Oktoba mwaka huu.
Kwa bahati nzuri au mbaya, sio wote tulio furahia
hatua hii kubwa iliyofanywa na msanii Kiba. Inasemekana msanii mkali wa Bongo
flava Tanzania, Diamond Platnums naye yupo nchini humo akijaribu kuiba SPOTLIGHT kwa kujaribu mbinu zote ili
aweze kupiga picha na neyo ili mradi aonekane kuwa naye alikuwepo.
Inasemekana Diamond alitua Nairobi Jumatatu
nakufikia kwenye Hoteli ya Hemingways
ambayo ndiyo Hoteli anayoishi Super Star huyo kutoka Marekani.
Waandaaji wa show hiyo ya Coke Studio
wamesema tayari wameshaweka ulinzi wakutosha wakum,zuia Diamond na crew yake
kupata “Photo Opportunity” na Ne-yo.
Picha aliyepost NE-YO katika ukurasa wake wa Instagram akiwa na King Kiba. |
No comments:
Post a Comment