Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt, ameshinda medali
yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea
mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt alitimuka mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55
na kunyakulia taifa lake medali nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa
mwanariadha kasi zaidi duniani katika mbio za masafa mafupi.
Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka
Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia.
Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya
fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa naGatlin
alitumia sekunde 19.74.
Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix
Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa
Bahamas akiridhika na medali ya fedha.
Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya
shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99.
Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada,
Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi
ya tatu kwenye mbio za mchujo.Hata hivyo Sum, alinusurika pale muda wake wa
dakika 1.57.56 ulikuwa wa kasi zaidi kati ya wale waliomaliza katika nafasi ya
tatu katika makundi yao, na hivyo kufuzu kwa fainali.
No comments:
Post a Comment