Serikali ya Kenya imetoa zawadi ya $20,000 wa mtu
yeyote atakaye toa habari za kukamatwa kwa mshukiwa mmoja wa ugaidi wa kike,
Rukia Faraj.
Idara ya polisi imesema kuwa Rukia anasakwa kwa
madai ya kuwasajili na kuwasafirisha watu wachanga kujiunga na mme wake nchini
Somalia kwa mafunzo ya ugaidi na pia kujiunga na kundi la kigaidi la Al
Shabaab.
Mume wake Ramadhan Kufungwa pia anasakwa na polisi
kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi nchini Kenya.Rukia sasa anajumuika na washukiwa wengine ambao
wanasakwa na serikali ya Kenya kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi.
Wengine ni pamoja na Mohammed Kuno anayejulikana kwa
jina la Gamadere au Dhuliadein ambaye anatuhumiwa kupanga mashambulio ya
kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa,ambapo zaidi ya watu 148 waliuawa.
SOURCE: Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment