Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amechaguliwa na muungano wa wanafunzi wa Vyuo vikuu barani Afrika AASU kama rais bora barani Afrika mwaka huu.
Muungano huo unasema kuwa maelfu ya wanafunzi kutoka kote
barani walishiriki katika kura hiyo.
Bwana Kenyatta alichaguliwa kwa uwezo wake wa kujenga
makubaliano kitaifa na kimataifa,juhudi zake za kubadilisha sera na kutoa
ufumbuzi katika maswala yanayowaathiri wakenya.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alishinda tuzo hiyo mwaka
uliopita.
SOURCE: Bbc Swahili
P.S: Tanzania nahisi tutachukuwa mwakani Inshallah ! hahaha
No comments:
Post a Comment