Mustafa Yussuf Suleyman, al maarufu kama “Smile The Genius”
ni msanii wa kizazi kipya wa Bongo Falva. Alianza Muziki rasmi mwaka 2005
Mbagala, mjini Dar_es_salaam ingawa alipata changamoto kubwa sana kutoka kwa
wazazi wake ambao hawakufurahia yeye kuingia katika tasnia ya Muziki.
Ilipofika Mwaka 2006
katika kuhangaika na maisha ya muziki ailifanikiwa kupata lebo katika studio
inayoitwa MAB J RECORDS iliyokuwepo Mwananyamala kwa Makoma.
“Haikuwa Rahisi kupata lebo studio hiyo kwa kabla niliambulia dharau, kashfa , unyanyasaji, matusi vyote ilifika Muda Nilitaka kukuata tamaa Lakini Mungu akawa ananipa nguvu ya kupigania kipaji changu”
Baada yakupambana kwa
dhati alikuja kufanikiwa kupata mkataba na Record
Label ya MAB J. Hapo alikutana
na wasanii wengi wakiwemo, Mirror, Diamond, na wengine wengi.
Mwaka 2010 kwa msaada
wa Uprise Music Studio chini ya Producer DUPPY na FRAGA Smile alifanikiwa
kurecord nyimbo kadha wa kadha ambazo hazikufanya vizuri sokoni , Mnamo mwaka 2012 alibahatika kutoa wimbo wa KICHEFUCHEFU CHA MOYO, wimbo uliompa
umaarufu nakumfanya kujulikana na wengi.
Mpaka sasa Smile ana
nyimbo tatu ambazo zimepokelewa vizuri sana na mashabiki zikiwemo Unazingua Video By NICK
DIZZO, Bei Nafuu ft Ommy Dimpoz Produced By KGT pamoja na Tujibanebane Produced By FRAGA.
P.S: Msanii huyu mara nyingi hufananishwa na msanii Platnums kwani wote wametoka Mbagala, wanasauti nzuri, mavazi yao, Swagg na kama vile miili yao inataka kufanana hivi. lol !
No comments:
Post a Comment