Jana nilitembelea Supermarket ya Nakumatt. Baada
yakumaliza kufanya manunuzi ya mahitaji yangu ya nyumbani (Shopping),
nilielekea kwa Cashier ili kufanya malipo. Chakushangaza, baada ya kulipia
groceries zangu niliambiwa nilipie na mfuko pia. Kitendo hichi kilinishangaza
sana hivyo basi nikaomba kupata ufafanuzi zaidi juu ya utaratibu huu mpya.
Muhudumu aliyenihudumia alionekana sii muongeaji na hakuwa na vigezo vya Customer care, hivyo
alinijibu kwamba. Ningependa kumnukuu
“Basi tuu ndiyo utaratibu mpya wa Nakumatt, Boss
ndokaamua”
Sikuridhishwa na jibu lake hivyo nilimfuata Manager
kutaka kujua, KUNANI ?
Kwa bahati nzuri au mbaya sikupata nafasi ya kuonana
na Manager kwa madai kuwa hakuwepo ofisini kwa muda ule.Ila nilifanikiwa
kuongea na administrator wa duka hilo na kuniambia kuwa , utaratibu huo wakuuza
mifuko ni agizo la serikali kupitia uongozi wa Manispaa kwamba kila Supermaket
inapaswa kuuza mifuko ili kupunguza uchafuzi wa mazingira .
Dada huyo
ambae hakupenda jina lake lijulikane aliendelea kufunguka nakusema kuwa
hata Supermarkets nyingine kama Game and
etc,wameshaanza kutekeleza zoezi hilo.
Je,
dukani kwa mangi pia tutauziwa mifuko ???
Unaonaje utaratibu huu upya ???
Haya wadau HABARI NDO HIYO !!! Sasa itakua mwendo wakubebana na mifuko kama zamani
No comments:
Post a Comment