South Carolina |
Polisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani
wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki amewapiga risasi na kuwaua watu
tisa ndani ya kanisa la kimethodist.
Polisi wa eneo hilo la Charleston wameelezea kuwa
kwa sasa wanamtafuta mshukiwa huyo anayeaminiwa kuwa kijana wa kizungu katika
miaka ya ishirini.
Shambulio hilo limefanyika ndani ya kanisa la
Emmanuel African Methodist Church, kanisa linaloaminiwa kuwa la zamani zaidi la
kiafrika nchini Marekani.
Polisi wamesema kuwa shambulio hili ni la chuki ya
rangi ya ngozi.
Polisi wakiangalia usalama nje ya Kanisa |
Waamini waungana kusali kwa pamoja kufuatia mauaji ya "Emanuel African Methodist Church" , South Carolina |
No comments:
Post a Comment